Friday, November 30, 2012

Uwindaji haramu wa Faru/Tembo


Uwindaji haramu dhidi ya Faru na Tembo umeelezwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa Barani Afrika. Hayo yamesemwa na Dk Joseph Okori ambaye ni Kiongozi wa Mpango wa kunusuru Faru kwa upande wa Afrika chini ya WWF.

Dk Okori alisema kuwa maelfu ya tembo na Farau takribani 588 wameuawa kwa kipindi cha mwaka huu wa 2012. “Faru wanaweza kupotea kabisa kwa kipindi cha miaka 10 kama hatutachukua hatua za kukomesha ujangili huo,” alisema Dk Okori.

Alisema kuwa nchini Afrika ya Kusini Faru wanauawa kila siku kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe zao. Dk Okori alieleza kuwa Asia ndiyo soko kubwa la pembe hizo za Faru  na hasa nchini Vietnam. Aliongeza kuwa kiasi kikubwa cha pembe za tembo zinasafirishwa kwenda nchini Thailand na China.
(source: http://wwf.panda.org/?206876/Only-10-years-left-to-save-rhinos)



No comments:

Post a Comment