Tembo/Elephants |
Friday, November 30, 2012
Uwindaji haramu wa Faru/Tembo
Uwindaji haramu dhidi ya Faru na Tembo umeelezwa kuongezeka
kwa kiasi kikubwa Barani Afrika. Hayo yamesemwa na Dk Joseph Okori ambaye ni
Kiongozi wa Mpango wa kunusuru Faru kwa upande wa Afrika chini ya WWF.
Dk Okori alisema kuwa maelfu ya tembo na Farau takribani 588
wameuawa kwa kipindi cha mwaka huu wa 2012. “Faru wanaweza kupotea kabisa kwa
kipindi cha miaka 10 kama hatutachukua hatua za kukomesha ujangili huo,”
alisema Dk Okori.
Alisema kuwa nchini Afrika ya Kusini Faru wanauawa kila siku
kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe zao. Dk Okori alieleza kuwa Asia ndiyo soko
kubwa la pembe hizo za Faru na hasa
nchini Vietnam. Aliongeza kuwa kiasi kikubwa cha pembe za tembo zinasafirishwa
kwenda nchini Thailand na China.
(source: http://wwf.panda.org/?206876/Only-10-years-left-to-save-rhinos)
(source: http://wwf.panda.org/?206876/Only-10-years-left-to-save-rhinos)
Maoni ya Katiba Mpya
Sophia Mateo Mkazi wa Bunju: Katiba ipige marufuku ubakaji wa watoto. Sophia Mateo a resident of Bunju: The Constitution should ban child rape |
Sophia Seme mkazi wa Bunju: Muungano wetu umekuwa mfano bora Barani Afrika, nataka uendelee kama ulivyo: Our union with Zanzibar has been a good example in Africa, I suggest it to remain as it is. |
Ally Chambuso mkazi wa Bunju: Wageni wasipewe maeneo ambayo wananchi wanakaa au kuyatumia: The Constitution should prohibit investors to be given the areas used by the citizen |
Mkazi wa Bunju akitoa maoni yake ya Katiba |
Mikidadi Likunguni |
Joseph Matonya |
Wakazi wa Kata ya Bunju wakifuatilia na kushiriki katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya. The residents of Bunju Ward are participating in the meeting of Constitutional Review Commission |
Saturday, November 24, 2012
Judge Joseph Warioba
Friday, November 23, 2012
Constitutional Review
Hamad: We need alternative imprisonment
Mbaraka Hamad (49) a businessman from Kisutu Ward in Dar es
Salaam, today he told the Commission of the
Constitutional Review that the new Constitution should stop the tendency of the
Tanzanian courts to imprison people with minor cases because it is expensive to
keep them. He said the cost of keeping one prisoner is about Sh 350,000 per
month.
Hamad suggested that the new Constitution should allow the
sentenced people to serve their punishments by reporting to the local
government officers. He said this is a better way to correct them and to reduce
congestion in prisons.
“We need the new Constitution to come up with alternative
sentences to people with such minor cases as stealing mangoes or chicken. There
is no need to send them into prison. The government spends so much money to
keep them. I suggest they should be given alternative imprison and they have to
report every day to the local government officers until they finish their punishment,”
said Hamad.
Wednesday, November 21, 2012
Vinyago vya chuma/Iron carvings
Maoni ya Katiba/Constitution
Tuesday, November 20, 2012
Monday, November 19, 2012
CCM WAPONGEZANA
Chama Cha Mapinduzi chajipanga kurejesha
imani kwa wananchi
Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam jana kimefanya mkutano mkubwa katika
viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwa nia ya kuipongeza Sekretarieti
mpya ya Chama hicho. Mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama wake kutoka Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni waliofika
kwa wingi walivifanya viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja kulipuka kwa shangwe ya
vigelegele, ngoma na nyimbo mbali mbali.
Waliopongezwa kupitia mkutano huo ni Rais Jakaya Kikwete
aliyechaguliwa tena kushika nafasi ya Uenyekiti wa Chama kitaifa na Philip
Mangula akiwa Makamu Mwenyekiti Bara. Dk Ali Mohamed Shein Makamu Mwenyekiti
Zanzibar. Wengine ni Abdulhaman Kinana alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu na Mwigulu
Nchemba Naibu Katibu Mkuu Bara, wakati Nape Nnauye alichaguliwa kuendelea na
nafasi yake ya Katibu Mwenezi wa Chama.
Rais Kikwete alisema Sekretarieti Mpya kwa kushirikiana na
wana CCM wote nchini wana wajibu wa kurejesha imani ya watanzania kwa Chama
hicho. Alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya tathmini ya kutosha na kuchukua
maamuzi ya kuhakikisha kuwa wananchi wanakiunga mkono CCM kama ilivyokuwa
zamani.
“Tunapaswa kufanya tathmini ni kujua nini Chama chetu
kimefanya mpaka kimekuwa na sura hiyo iliyokuwa nayo sasa kwa jamii. Tutafute
sababu ili kuwafanya wananchi waweze kukiunga mkono tena,” alisema Rais
Kikwete.
Pia ameitaka Sekretarieti hiyo kufanya mikutano ya hadhara
na mikutano ya ndani kama mkakati wa kujijenga upya. Aliwataka kuzunguka nchi
nzima na kuzungumza na wanachama na wananchi ili kurejesha tena imani ya
wananchi kwa CCM.
Naye Makamu Mwenyekiti, Philipo Mangula alisema kuwa yeye
kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama hicho atahakikisha ndani ya miezi
sita wala rushwa na watoa rushwa watashughulikiwa vyema ili kukisafisha Chama.
Alisema wote ambao wamepata uongozi kwa njia ya rushwa hawataachwa salama na
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Tutashughulikia malalamiko yote ndani ya miezi sita. Wote
walioingia madarakani kihalali hao
wataendelea lakini wale waliotumia rushwa hatutasubiri polisi au Takukuru, hao
hawataendelea ni lazima tuwatoe nje ya uongozi. Mlima nyanya kurudi kazini basi
juje ipo kazi,” alisisitiza Mangula.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdulahaman
Kinana alisema kuwa majukumu waliyonayo ni kuisimamia Serikali. Alisema Chama
hakiwezi kutimiza wajibu huo ikiwa kuna rushwa, upendeleo na mizengwe. “Kuna
tatizo la mmomonyoko wa maadili ndani ya Chama. Hatuwezi kusimamia uadilifu
kama sisi wenyewe siyo waadilifu. Tutasimamia katiba yetu, kanuni na
maelekezo ya vikao vizuri,” alisema
Kinana.
Alisisitiza kuwa uongozi ndani ya Chama siyo ajira ila ni
kujitolea. Alisema kuwa kukijenga Chama ili kukirudishia heshima kama
ilivyokuwa awali.
Friday, November 16, 2012
Msiba wa Mzee Venant Hinju
Wednesday, November 14, 2012
Mahubiri/Preachings
Waumini wakiimba kwa furaha/ Chirstian are joyfully singing during the mass |
Tuesday, November 13, 2012
Taka taka kila mahali/ Filth everywhere
Sunday, November 11, 2012
Mkutano wa GNLD/ GNLD Meeting at Ubungo Plaza
Waalikwa/Invitees
Maelezo kwa wageni
Saturday, November 10, 2012
Police wakidhibiti wananchi
MV KIGAMBONI
Thursday, November 8, 2012
Miraculous Stone
DATA Center Training in Dar es Salaam
IDCA Lecturer
Monday, November 5, 2012
Wanaume Kazini/ Men at work
Saturday, November 3, 2012
TBS Essay Participants/Washiriki
Ngoni People dance Lizombe
Maji Maji Heroes
Subscribe to:
Posts (Atom)