Monday, December 17, 2012

MAITI YA MTOTO YAOKOTWA

Wakazi wa Mabibo Farasi Jijini Dar es Salaam wakiangalia kwa hudhuni maiti ya mtoto mchanga aliyetupwa pembeni ya mfereji wa maji unaopita eneo hilo siku ya Jumamosi. Kifo cha mtoto huyu anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 5 kinadhaniwa kusababishwa na utoaji mimba. Polisi walifika na kuuchukua huku muhusika akiendelea kusakwa. The residents of Mabibo Farasi in Dar es Salaam are looking at the body of a child of about 5 months old. Her death is associated with abortion. The police officers collected the body.

Hivi ndivyo haki ya kuishi inavyokiukwa. That is how the right to life is violated.

JOHN MNYIKA/CHADEMA MP FROM UBUNGO

Mbunge wa Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Amewaambia kuwa maana ya Nguvu ya Umma ni kuutumikia umma na siyo kuutumikisha umma. The Ubungo MP John Mnyika is addressing CHADEMA Members at public meeting at Kijitonyama in Dar es Salaam yesterday. He told people that Peoples' Power slogan aims at serving people not otherwise.





MKUTANO WA CHADEMA/CHADEMA MEETING

Kijana akichezea na moto kwenye  mkutano wa Chadema uliofanyika jana kwa Alimau 'A' Jijini Dar es Salaam. The young man is playing with fire in Dar es Salaam when Chadema held their meeting at Kijitonyama yesterday.

Akishika moto kwa mikono kwa staili ya kuunawa. He is touching fire with his  hands.

Mchezo ukiendelea. The show continues.

Ameuweka moto mfuko wa nyuma wa kaptura yake.  He put the burning fire on his back

Mambo hayo unayaweza? Don't try its risky







Ameamua kuula kabisa moto wake. At last he decided to eat it.

Thursday, December 13, 2012

Magari ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yakiwa yamepaki kwenye viwanja vya shule ya msingi Makuburi. Leo Tume ilikuwa ikichukua maoni ya wakazi wa kata ya Makuburi

Monday, December 10, 2012

WAKAZI WA MABIBO/MABIBO RESIDENTS

Dk Salim Ahmed Salim akizungumza na wakazi wa Kata ya Mabibo Jijini Dar es Salaam. Amewataka wananchi kuepuka ushabiki wa kidini au kisiasa katika kutoa maoni yao. Dr Salim Ahmed Salim talks to the Mabibo residents; He wanted them to avoid religious and or political  fanaticism in their opinion

Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume akiwapatia katiba na vipeperushi wanafunzi wa Sekondari ya Loyola.

Kurusumu Peter akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Twahili Mwinyi Mkuu akishiriki kutoa maoni yake ya Katiba

Wakazi wa Mabibo wakishiriki kutoa maoni yao ya katiba

Friday, December 7, 2012

Wakazi wa Kata ya Manzese Jijini Dar es Salaam

Abdullah Hamisi: Sherehe za mitaani pamoja na baa vinaharibu maadili ya watoto, Katiba ipige marufuku. The new constitution has to prohibit night celebrations in our streets, they are the source for ethical violation to our children

Yahya Ndyema: Serikali, Bunge na Polisi wanaongoza kuvunja haki za binadamu nchini, Katiba iwalinde wananchi. The government, the Parliament and the Police Force are greatly violating human rights; I suggest the new constitution has to stop it.

Wakazi wa Kata ya Manzese Jijini Dar es Salaam wakishiriki kutoa maoni yao. The residents of Manzese in Dar es Salaam are participating in constitutional review meeting.

Wakazi wa Manzese wakifuatilia kwa karibu utoaji wa maoni ya katiba mpya. Manzese residents are closely making a follow up to the constitutional review meeting.

Wakazi wa Manzese wakishiriki kutoa maoni ya katiba kwa njia ya maandishi. Some residents of Manzese are offering their opinion in writing

Wakazi wa Manzese wakifuatilia utoaji maoni. Manzese residents

Wakazi wa Kata ya Makongo-Dar es Salaam

Ritha Mboto: Katiba ipige marufuku neno umasikini kwani Tanzania ni nchi tajiri. The New Constitution has to ban the word poverty in this country, Tanzania is not a poor country

Gertrude Mongella: Haki za watoto ziheshimiwe na kulindwa kikatiba. Wazazi wanaotelekeza watoto wao wadhibitiwe kisheria. The rights of children must be respected and protected in the coming constitution. The parents who abandon their children should  be punished according to the law

Deus Mtiro: Ajira kwa wageni zipigwe marufuku, wazawa wapewe kipaumbele kwanza. Foreigners should not be given the first priority in employment, let the indigenous be the first.

Wakazi wa Kata ya Makongo wakisubiri kutoa maoni yao. The residents of Makongo Ward in Dar es Salaam are waiting to offer their opinion

Wakazi wa Kata ya Makongo wakifuatilia utoaji wa maoni ya Katiba Mpya. The Makongo residents.

Wednesday, December 5, 2012

Wananchi wa Dar es Salaam wakitoa maoni yao ya katiba

Wakazi wa Sinza wakitoa maoni yao katiba.

Wakazi wa Sinza wakifuatilia kwa makini utoaji wa maoni

Wasanii wakitumbuiza kwenye mkutano wa katiba katika kata ya Saranga Jijini Dar es Salaam

Maji yakipotea hovyo kutokana na kupasuka kwa bomba karibu na ofisi za Kata ya Saranga

Mwalimu Sophia Mshanga: Kuwe na idadi maalumu ya wizara

Sunday, December 2, 2012

Redds Miss Tanzania: Brigitte Lymo

Brigitte Lymo  Kawe resident: Katiba Mpya iwalinde Albino na walemavu wote. The New Constitution has to protect Albino and other disabled people.

Wakazi wa Kawe/Kawe Residents

Abdi Hamisi: Nataka Muungano wa mkataba

Germinus Nyeho: Kiswahili iwe lugha ya kufundishia kwenye shule na vyuo vyote nchini

Esther Mkwizu M/kiti Tume: Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83 inawataka wananchi kutoa maoni yenu kwa uhuru, msiwe na hofu

Wakazi wa Kata ya Kawe Jijini Dar es Salaam wakishiriki kutoa maoni yao

Sharifa Ngogoro: Katiba ilinde haki za wanawake kwenye suala la mirathi, wanaonewa sana

Vicent Mayunga: Polisi wanafanyakazi za ajabu, wananyanyasa wananchi, Katiba iliangalie suala hilo

Friday, November 30, 2012

Tembo/Elephants

Tembo/Elephants

Uwindaji haramu wa Faru/Tembo


Uwindaji haramu dhidi ya Faru na Tembo umeelezwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa Barani Afrika. Hayo yamesemwa na Dk Joseph Okori ambaye ni Kiongozi wa Mpango wa kunusuru Faru kwa upande wa Afrika chini ya WWF.

Dk Okori alisema kuwa maelfu ya tembo na Farau takribani 588 wameuawa kwa kipindi cha mwaka huu wa 2012. “Faru wanaweza kupotea kabisa kwa kipindi cha miaka 10 kama hatutachukua hatua za kukomesha ujangili huo,” alisema Dk Okori.

Alisema kuwa nchini Afrika ya Kusini Faru wanauawa kila siku kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe zao. Dk Okori alieleza kuwa Asia ndiyo soko kubwa la pembe hizo za Faru  na hasa nchini Vietnam. Aliongeza kuwa kiasi kikubwa cha pembe za tembo zinasafirishwa kwenda nchini Thailand na China.
(source: http://wwf.panda.org/?206876/Only-10-years-left-to-save-rhinos)



Maoni ya Katiba Mpya

Sophia Mateo Mkazi wa Bunju: Katiba ipige marufuku ubakaji wa watoto. Sophia Mateo a resident of Bunju: The Constitution should ban child rape

Sophia Seme mkazi wa Bunju: Muungano wetu umekuwa mfano bora Barani Afrika, nataka uendelee kama ulivyo: Our union with Zanzibar has been a good example in Africa, I suggest it to remain as it is.

Ally Chambuso mkazi wa Bunju: Wageni wasipewe maeneo ambayo wananchi wanakaa au kuyatumia: The Constitution should prohibit investors to be given the areas used by the citizen

Mkazi wa Bunju akitoa maoni yake ya Katiba

Mikidadi Likunguni

Joseph Matonya

Wakazi wa Kata ya Bunju wakifuatilia na kushiriki katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya. The residents of Bunju Ward are participating in the meeting of  Constitutional Review Commission