Monday, July 15, 2013

MAJAMBAZI WATEKA MABASI BIHARAMULO

Majambazi wapatao 10 wameyateka mabasi mawili ya kampuni za RS na NBS leo alfajiri na kuwapora abiria mali na fedha, pia askari aliyekuwa akiyasindikiza mabasi hayo naye ameporwa bunduki aliyokuwa nayo SMG namba 14302551; Kamanda Philip Kalangi (RPC) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Thursday, March 14, 2013

PAPA MPYA/NEW POPE

Kardinali Jorge Bergoglio kutoka Argentina amechaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki Duniani. Jina lake la Kichungaji ni Papa Francis I. Cardinal Jorge Bergoglio from Argentina has been elected the New Pope of the Catholic Church. He will be called Pope Francis I.

Friday, February 8, 2013

Road Accident

Lorry likishindwa kupanda mlima Mkoani Ruvuma kutokana na mafuta kumwagika kwa wingi bara barani.

Friday, February 1, 2013

Graduation/Mahafali


Editha Expedito akiwa kwenye sherehe ya kuhitimu elimu ya chekechea akijiandaa kuingia darasa la kwanza mwaka 2013. Editha Expedito has finished her
Nursery studies now she prepares for Standard 1 Education next year, 2013

Katiba/Constitution

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Loyola wakipewa fomu ili watoe maoni yao Katiba Mpya. Stundents from Loyola Secondary School are being given special form by a Member of Constitutionl Review Commission so that they may fill in their opinion

Tuesday, January 15, 2013

WAKUU WA MIKOA

Wakuu wa Mikoa wakibadilishana mawazo mara baada ya kutoka kutoa maoni yao ya Katiba Mpya kwenye Makao Makuu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akiwaeleza Waandishi wa Habari kuwa wamependekeza Tume izingatie kuyafanyia kazi maoni yote Watanzania waliyoyatoa ya Katiba Mpya

Saturday, January 12, 2013

DEUS KIBAMBA

Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi, Deus Kibamba akieleza namna Katiba inavyoweza kuboresha uhuru wa kupata habari kwa wananchi na vyombo vya habari.



MAKUNDI MAALUMU KATIBA

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Severine Niwemugize wa Jimbo Katoliki la Rulenga-Ngara akiwaeleza waandishi wa habari kuwa Ubalozi wa Vatican kuwepo hapa nhcini ni halali kwa kuwa Vatican ni nchi kamaili ndani ya Italia. The Deputy President of Tanzania Episcopal Conference, His Lordship Bishop of Rulenge-Nghara Severine Niwemugizi told journalists yesterday in Dar es Salaam that it is the right for the Pope's Ambassador to be in Tanzania because Vatican is an independent country within Italy.

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akibadilishana mawazo na Mh Andrew Chenge nje ya viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuwasilisha maoni yao ya Katiba Mpya. Hon Kingunge Mwiru and Hon Andrew Chenge exchange ideas at Karimjee after they had presented their opinion on the New Constitution.

Mwenyekiti, Wajumbe wa Tume ya Katiba wakiwa kwenye picha ya ukumbusho na Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila kwenye Makao ya Tume ya Katiba